Follow by Email

Friday, October 14, 2011

NYERERE NAKULILIA

NYERERE NAKULILIA!

Nyerere unanisikia?
Machozi nakulilia
Nchi ulopigania
Uhuru Kutuachia.

Nchi ulopigania
Ukajenga Historia
Vigogo ukawachia
Tumebaki tukilia

Ufisadi, umezidia
Na uchafu kupindukia
Mali wajilimbikia
Mafukara tunalia

Mafukara tunalia
Twaililia Tanzania
Nini wanafurahia?
Kama wengi tunalia?

Kwa mbebwe,uongo pia
Bungeni wakaingia
Nini wametufanyia?
Kama vile si raia!

Mikataba kusainia
As if hawana nia
Sisi kutusaidia
Nyerere nakulilia

Kuna Haja Tanzania
Kutafuta zote njia
Fisadi, wababe pia
Kila njia kutumia

Kila njia kutumia
Siyo tu kulialia
Haki yetu kutumia
Kuichange Tanzania!

Nyerere Nakulilia
Copyright@ Kahabi Isangula, 14th October 2011

No comments:

Post a Comment